Ngoma Asajiliwa Aza Fc, Kumbe Hakuwa Anaumwa
Rasmi uongozi wa Azam FC umethibitisha kuingia mkataba wa mwaka mmoja na aliyekuwa mchezaji wa Yanga, Mzibambwe, Donald Ngoma.
Ngoma amejiunga na Azam baada ya kusitishiwa mkataba wake na Yanga kutokana na kuwa majeruhi wa muda mrefu hivyo kushindwa kugharamika juu ya matibabu yake.
Ngoma alishindwa kukitumikia kikosi cha Yanga kwa takribani msimu mzima wa 2017/18 kutokana na hali yake kiafya kutoruhusu kucheza hivyo kuendelea kuwa nje ya kikosi.
Azam sasa watagharamika kwa ajili ya matibabu ya mchezaji huyo ambaye mpaka sasa ni majeruhi, na taarifa zinaelezwa kuwa watampelekea Afrika Kusini kufanyiwa vipimo vya afya.
Ngoma alijiunga na Yanga akitokea FC Platnum ya Zimbambwe mnamo mwaka 2015 wakati huo Mfanyabiashara, Yusuph Manji akiwa Mwenyekiti wa klabu hiyo.
No comments: