Simba Inahitaji Point Moja Tu Kutangaza Ubingwa VPL
Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea Jumapili ya May 6 2018 kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja mbalimbali Tanzania bara, mchezo kati ya Simba dhidi ya Ndanda FC uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Simba ambao wanatajwa kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji msimu huu kuliko vilabu vingine leo wamefanikiwa kupata point tatu kwa ushindi finyu wa goli 1-0 goli ambalo lilifungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 44.
Goli hilo kwa upande wa Emmanuel Okwi linakuwa ni goli lake la 20 msimu huu akiwa amebakiza magoli 2 kuivunja rekodi ya Amissi Tambwe aliyewahi kuibuka mfungaji bora wa VPL kwa kufunga jumla ya magoli 21.
Kwa upande wa Simba ushindi wa leo umewafanya wafikishe jumla ya point 65 akihitaji point moja tu kuwa Bingwa wa VPL msimu huu kwani watakuwa wamefikisha jumla ya poiny 66 ambazo zitakuwa haziwezi kufikiwa na timu yoyote lakini Simba imebakiwa na michezo mitatu dhidi ya Singida, Majimaji na Kagera Sugar ila ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo msimu huu.
No comments: