Mchungaji auawa na Mamba akibatiza
Nakusogezea stori kumhusu Mchungaji Docho Eshete ambaye ameuawa na mamba alipokuwa akiwabatiza waumini wake katika ziwa Abaya nchini Ethiopia.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa mamba huyo aliibuka kwenye maji na kuanza kumshambulia mchungaji Eshete miguuni, mikononi na mgongoni.
Mchungaji huyo alifanikiwa kumbatiza muumini mmoja tu kabla mamba hajaharibu zoezi hilo.
Hata hivyo wavuvi na wakazi wa eneo hilo walijitahidi kumuokoa mchungaji huyo mdomoni mwa mwamba lakini jitihada zao hazikuzaa matunda huku mamba huyo akifanikiwa kutoroka.
No comments: