Header Ads

ad

WALICHOBAINI POLISI BAADA YA KUMKAMATA MNUNUZI FEKI WA NYUMBA ZA LUGUMI


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamtuhumu Dk. Louis Shika, kutumiwa na mfanyabiashara Said Lugumi, ili kukwamisha uuzwaji wa nyumba zake zinazoshikiliwa na serikali.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ameeleza wanatilia shaka kuwa mtuhumiwa alitumwa na Lugumi kukwamisha mchakato wa mnada, kwani mazingira ya mnada, na namna mtuhumiwa aliyokuwa anataja bei yanawafanya kuamini kuwa aliwekwa ili wanunuzi wengine wasiweze kununua nyumba hizo.

“Aliwekwa na Lugumi mwenyewe ili mnada usifanyie ingawa sina fact za kudhibitisha hilo, ila alichokuwa anakifanya kinatufanya tuamini hivyo. Alikuwa ana top bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,” amesema Mambosasa.

“Ila jinsi alivyo, kwa maana ya uvaaji na kuongea kwake watu walitia mashaka kama ataweza kununua ndipo akatakiwa kutoa asilimia 25 na kushindwa kulipa. Tunaendelea kumshikilia kwa mahojiano,” aliongeza.

Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia Dk. Louis kwa mahojiano zaidi na pale upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani ili kuchukuliwa hatua za kisheria.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.