Header Ads

ad

Hakimu Agoma Kujitoa Kesi ya Abdul Nondo

Hakimu John Mpitanjia anayesikiliza kesi ya kujiteka na kusambaza taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii, inayomkabili Abdul Nondo, amegoma kujitoa katika kesi hiyo kwa sababu za kumkataa ni za kufikirika na hazina mashiko.

Mei 14 mwaka huu, mshatakiwa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), aliandika barua ya kumkataa hakimu huyo kujitoa kutokana na kutokuwa na imani naye ambapo alitoa sababu tano akidai ukaribu wake na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Iringa na shahidi wa tatu katika kesi hiyo, Paul Kisapo unatia shaka.

Akitoa uamuzi huo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa,  Hakimu Mpitanjia amesema sababu alizotoa mshtakiwa hazina msingi wowote na ataendelea kusikiliza shauri hilo kwani akijitoa haki itachelewa.

Akizungumzia uamuzi huo wa mahakama, Wakili wa Nondo, Jebra Kambole, amesema upande wa utetezi wamepokea uamuzi wa mahakama na hawawezi kuupinga ila kama kutakuwa kuna ulazima wa kufanya jambo lolote la kisheria watatumia njia nyingine za kupata haki yao.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.